Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Boric, Rais wa Chile, katika hotuba kali huko New York, alilaani vikali serikali ya Israel na kukumbusha kuwa: “Maelfu ya watu wasio na hatia wanapoteza maisha yao kwa kosa pekee la kuwa Wapalestina, Ghaza ni janga la kimataifa kwa sababu ni janga la kibinadamu.”
Akasema kwa kusisitiza: “Sitaki Netanyahu pamoja na familia yake waangamizwe kwa kombora. Nataka Netanyahu na viongozi wanaohusika na mauaji ya kimbari dhidi ya taifa la Palestina wasimame mbele ya mahakama ya kimataifa ya haki.”
Uhusiano baina ya Chile na Palestina ni wa kihistoria. Wapalestina wanaokadiriwa kufikia nusu milioni wanaishi Chile, jambo linaloifanya jamii ya Kipalestina nchini humo kuwa kubwa zaidi kati ya Waarabu nje ya Mashariki ya Kati Chile tangia mwaka 2011 ililitambua rasmi taifa la Palestina na ikaunga mkono uanachama wake katika UNESCO.
Mwezi Novemba 2023, Boric alimrejesha balozi wa Chile kutoka Tel Aviv, ingawa kiwango cha uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili hakikupunguzwa rasmi.
Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Afya ya Ghaza, ambayo tangu mwaka 2007 ipo chini ya udhibiti wa Hamas, takriban Wapalestina 65,062 — wengi wao wakiwa raia — wamepoteza maisha yao kutokana na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Ghaza.
Maoni yako